Sh bilioni 1 kujenga sekondari Dinyecha

SERIKALI imetoa zaidi ya Sh bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Dinyecha iliyopo Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani mtwara.

Shule hiyo ni kwa ajili ya kidato cha tano na sita ambayo inayotarajia kupokea zaidi ya wanafunzi 500 baada ya kukamilika kwake.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Nasibu Ally amesema ujenzi huo unahusisha madarasa 18, mabweni 6, matundu ya vyoo 35 huku akieleleza changamoto iliyokuwa ikiukumba mradi hapo awali ikiwemo suala la maji lakini kwa sasa changamoto hiyo imefanyiwa kazi.

Advertisement

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota ameridhishwa na kasi ya ujenzi kwani majengo yako kwenye ubora unaotakiwa.

‘’Hali iliyopo sasa hivi isipowe yaani iendelee hivi hivi mpaka itakapofika Agosti tukamilishe ujenzi wetu kwa wakati hatimaye wanafunzi waingie madarasani itakapofika Agosti 13 mwaka huu nimefurahishwa sana na kasi ya ujenzi.

”Amesema Chikota.

Moza Subri mkazi wa Kibaoni katika halmashauri hiyo, amesema ujenzi wa shule hiyo ni furaha kubwa kwake na wananchi wenzake kwa ujumla kwani umewapunguzia gharama ya watoto wao kwenda nje ya halmashauri yao kufata elimu ya kidato hicho tano na sita.

‘’Tunaishukuru sana serikali kwa kutujengea karibu shule hii ya kidato cha tano na sita na shule kubwa kama hii ambayo itachukuwa watoto wengi haijawahi kutokea ni shule ya kwanza kwenye maeneo yetu na itaturahisishia kusomesha watoto wetu kwa karibu na itatupunguzia gharama ya kusomesha watoto mbali na hapa mana wengi wetu hali vipato vyetu kimaisha ni vya chini.”amesema Subri.

Ujenzi huo ulianza Juni mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *