Sh bilioni 93.09 kuendeleza ujenzi wa daraja Kigongo-Busisi

TAKRIBANI Sh bilioni 93.09 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi (Mwanza) ambao umefikia asilimia 63.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma leo, Majaliwa amesema kukamilika kwa daraja hilo kutapunguza muda wa wananchi kuvuka eneo la Kigongo – Busisi kutoka saa 2 mpaka dakika 4 kwa kutumia usafiri wa gari na dakika 10 kwa watembea15 kwa miguu.

Majaliwa amesema daraja hilo litakuwa na uwezo wa kupitisha magari ya aina yote wakati wote na kubeba uzito wa hadi tani 160.

Habari Zifananazo

Back to top button