Sh milioni 500 kuboresha huduma ya maji Nkasi

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewahakikishia Wananchi wa kijiji cha Palamawe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa fedha za kuboresha mtandao wa maji zipatazo Sh milioni 500.

Akizungumzia changamoto ya maji baada ya kusikiliza kero za Wananchi waliosema maji kwa sasa hayatoshelezi kwa sababu mradi uliopo umekuwa wa muda mrefu, Chongolo ameahidi kufuatilia ili fedha hizo zilizotajwa kuhitajika kutekeleza mradi huo zipatikane. Ametaka kata zenye uhaba wa maji ni Myula na Kate.

“Nimesikia hapa inatakiwa tutafute fedha kama milioni 500 ili kuboresha mtandao wa upatikanaji maji. Mtalaamu anasema tukipata Sh milioni 500 mtandao wa maji kwa hizi kata mbili utaboreshwa na utatoa maji vizuri, sasa nalichukua hilo la kwenda kuboresha mtandao wa maji hapa.”amesema Chongolo.

Chongolo, ameingia Mkoa wa Rukwa, akitokea Katavi akiendelea na ziara yake ya kukagua uhai wa chama,sambamba na kusikiliza kero za wananchi. Aidha,ziara hiyo iinaangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020 – 2025.

Kuhusu miundombinu ya barabara, Chongolo ametumia nafasi hiyo kumsimamisha Meneja Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) mkoani humo ili kutoa maelezo kuhusu hatua zinazochukuliwa kuboresha barabara ambazo zimelalamikiwa na wananchi kuwa hazipitiki nyakati zote.

“Mwaka 2013 nilikwenda Wampembe wakati ule ilikuwa anasa , nilikwama njiani karibu mara nne, nikafika wampembe tuko hoi taabani lakini baada ya hapo kiongozi niyekuja naye wakati huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM aliahidi kuleta sh milioni 500 ili barabara ile ifunguliwe na baada ya miezi mitatu fedha ililetwa na barabara ilifunguliwa sasa hivi inapita lakini inahitaji marekebisho maeneo korofi.

“Lakini barabara nyingine ni barabara ya Mpanda- Nkala ambayo nayo inahitaji marekebisho na barabara ya tatu ni Kibombe-Nkasi,”amesema Chongolo wakati akielezea changamoto ya barabara hizo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi.

Hata hivyo Meneja wa TARURA amesema kila mwaka wamekuwa wakifanya maboresho ya barabara zote korofi kwa kuweka zege katika maeneo ya vilima vikali pamoja na makaravati.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
UCHANGUZI LEO
UCHANGUZI LEO
1 month ago

NEC UCHANGUZI LEO

Nani anafaa KUWA RAIS wa Tanzania mzungu kulipa fadhila za OBAMA KUWA RAIS WA MAREKANI NA Greg Fergus SPIKA WA CANADA WA SASA!? – Hongera kwa kuzaa kizazi kisichojihusisha na SIASA…
 
MAANA YAKE NI KUCHAGUA RAHA ZA IDI AMINI DADA ILI WATOTO WAZILITHI!

Work AT Home
Work AT Home
Reply to  UCHANGUZI LEO
1 month ago

Earn money in USA, high scores from trusted resources. Work at your own pace. Regular Payments. Search in different job categories. Work anywhere on your vs03 computer, laptop or mobile phone. Update your profile at any time.
.
.
Detail Here———->>> http://Www.Smartcash1.com

UCHANGUZI LEO
UCHANGUZI LEO
1 month ago

NEC UCHANGUZI LEO

Nani anafaa KUWA RAIS wa Tanzania mzungu kulipa fadhila za OBAMA KUWA RAIS WA MAREKANI NA Greg Fergus SPIKA WA CANADA WA SASA!? – Hongera kwa kuzaa kizazi kisichojihusisha na SIASA…
 
MAANA YAKE NI KUCHAGUA RAHA ZA IDI AMINI DADA ILI WATOTO WAZILITHI!

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x