Sh milioni 800 kutolewa mikopo wajasiriamali Kigoma Ujiji

KIGOMA: HALMASHAURI Manispaa ya Kigoma Ujiji inatarajia kutoa Sh milioni 800 mkopo kwa vikundi 71 vya wajasiriamali na wafanyabiashara ndogondogo ili kukuza biashara zao.

Mkuu wa Wilaya Kigoma, Dk Rashid Chuachua amesema hayo wakati Benki ya CRDB kupitia programu ya utoaji mikopo ya asilimia 10 kutumia mfumo jumuishi (imbeju) inayosimamiwa na CRDB Foundation ilipokabidhi Sh nilioni 63.5 kwa vikundi vinane vya wajasiriamali wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Wilaya Kigoma, Mganwa Nzota amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa kuwezesha idadi kubwa ya wananchi wa manispaa hiyo kufanya biashara zao kwa tija kubwa ili kuimarisha uchumi wa familia zao.

Dk.Chuachua amesema kuwa mikopo hiyo ambayo haina riba inalenga kuwaondoa watu wa makundi maalum kwenye changamoto ya kuchukua mikopo yenye riba kwenye taasisi binafasi zinazotoa mikopo ambazo pamoja na kuwa na riba kubwa ambazo zimesababisha wajasilimali kurudisha mikopo lakini pia mali na bidhaa zao zimekuwa zikikamatwa na kutaifishwa na taasisi.

Katibu Tawala wa Wilaya Kigoma Mganwa Nzota (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 63.5 kwa viongozi wa vikundi vinane vya wajasiliamali wa manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akizungumza katika utoaji mikopo hiyo Meneja wa CRDB Bank Foundation, Fadhili Bushagama alisema kuwa vikundi vinane vinapatiwa mikopo hiyo yenye thamani ya Sh milioni 63.5 baada ya kukidhi vigezo na michakato mbalimbali iliyofanyika kutafuta vikundi hivyo.

Bushagama amesema kuwa katika mchakato huo vikundi 18 vilitembelewa kufanyiwa mchakato wa kujua uendeshaji wa biashara zao, utunzaji wa hesabu, taratibu nzuri za utunzaji wa fedha na taratibu nzuri za taarifa ya biashara na hivyo kufanikiwa kupata mikopo hiyo na kwamba vikundi 98 viliainishwa awali vikiomba mkopo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button