Sh Tri.1.6 kutekeleza vipaumbele vya afya

DODOMA; WIZARA ya Afya imewasilisha bajeti ya Sh 1,618,191,235,000.00 ili ni kuweza kutekeleza malengo na vipaumbele iliyojiwekea kwa mwaka 2025/26.
Kauli hiyo imetolewa bungeni na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026.
“Mheshimiwa Spika, Kiasi cha Shilingi Trilioni moja, Bilioni mia sita kumi na nane, milioni mia moja tisini na moja, laki mbili na elfu thelathini na tano (1,618,191,235,000.00) kimekadiriwa kutumika kutekeleza vipaumbele hivyo na afua mbalimbali,” amesema.



