MREMBO Mtanzania Sharon Julius ameiwakilisha vyema Tanzania baada ya Julius kuibuka mshindi wa pili ‘1st runner-up’ katika mashindano ya Miss Africa International 2024 yaliyofanyika Accra nchini Ghana.
Miss Africa International ni shindano linalojikita katika ushawishi wa utalii, utamaduni na ujasiriamali hata hivyo limeshirikisha warembo kutoka mataifa mbalimbali Afrika.
Mshindi wa taji hilo mwaka huu ni Tamunosoye Karibi George kutoka Nigeria na nafasi ya tatu ‘2nd runner-up’ imeenda kwa Marineth Medina raia wa Angola.
Mshindi wa Taji la Miss Africa International 2023 alikuwa Nazimizye Adam kutoka Tanzania.
Kitaaluma Sharon ni muuguzi na mkunga, na pia ni mwanaharakati anayejikita katika kupunguza idadi ya vifo vya watoto njiti Tanzania kupitia elimu na programu za mafunzo.