Sheria yatoa mwongozo kampeni za Uchaguzi Mkuu

DODOMA :WAGOMBEA katika Uchaguzi Mkuu wameelekezwa kuwasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi mapendekezo ya ratiba inayoonesha muda na mahali mikutano ya kampeni itakapofanyika.

Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya 2024 inaeleza kampeni za uchaguzi zitaendeshwa na mgombea, chama na wakala wake. SOMA: Mgombea kuomba kura kwa Whatsapp, TikTok, Facebook

Kwa mujibu wa sheria hiyo mgombea, wakala na chama wanapaswa kuwasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi mapendekezo ya ratiba inayoonesha mpangilio unaopendekezwa kufanya mikutano ya hadhara ya kampeni inayoainisha muda na mahali mikutano itakapofanyika. Pia, kupitia Kifungu cha 73 (4) anatakiwa kupitia ratiba za kampeni na wagombea wa vyama vyote.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button