Shule jumuishi ya mfano yazinduliwa Mtwara

SERIKALI imezindua shule jumuishi ya Msingi ya kwanza ya mfano nchini kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu nchini.

Shule hiyo ya Lukuledi iliyopo  katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara,ilizinduliwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Amesema shule hiyo imejengwa na Wizara hiyo kupitia mradi wa kuendeleza ujuzi nchini (ESPJ).

“Shule hii ya Jumuishi ya Msingi ni ya kwanza ya mfano ambayo huwezi kuiona sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania kwa usawa, wingi wa miundombinu na kutoa mahitaji yote kwa wanafunzi wote wenye mahitaji maalumu,” amesema.

 

Profesa Mkenda amesema shule hiyo haina mfano Tanzania nzima, ina miundombinu ya kutosha kukidhi mahitaji yote ya watoto wenye mahitaji maalumu.

Ametaja baadhi ya miundombinu hiyo kuwa ni mabweni yenye vyumba maalum vya kipekee (self-contained) kwa wanafunzi wenye ulemavu wa viungo ambao wanatumia wheelchairs.

Miundombinu mingine Maalumu kwenye shule hiyo ni chumba maalumu kwa ajili ya kupima usikivu kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Shule hiyi pia ina karakana sita ikiwemo karakana ya magari, ushonaji , saluni kwa ajili ya kutoa mafunzo stadi kwa wanafunzi.

Amesema ujenzi wa shule hiyo ambayo imegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja ni kutokana na juhudi za Raisi Dk Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha watoto wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu wanaandikishwa, wanafundishwa na kupata elimu kukamilifu.

Habari Zifananazo

Back to top button