Siku ya wanawake itumike kupinga ukatili-CCM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ltifaki na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Sophia Mjema amesema katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hapo kesho,itumike kuhimiza jamii kuacha vitendo vya ukatili kwa kundi hilo na badala yake itumike kuhamasisha jamii kusomesha watoto wa kike.

Kauli hiyo ameitoa leo Katika Kijiji cha Sarame wilayani Babati katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo mkoani Manyara akikagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya 2020/25 na kukagua uhai wa chama hicho mashinani na kuzungumza na makundi mbalimbali.

“Kesho ni Siku ya Wanawake Duniani,tuiazimishe kwa kutoa elimu kwa jamii kuacha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto na tuitumie kuhimiza jamii kusomesha watoto hususan wa kike”,amesema Mjema.

Advertisement

Aidha amewataka maafisa kilimo kufika kwenye maeneo ya wananchi vijijini na kuwaelimisha kuacha kulima kwenye milima na kukata miti kunakosababisha nyakati za mvua mafuriko kutokea maeneo tambarare.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *