WAZIRI wa Habari, Mawasliano na Teknoloja ya Habari, Jerry Silaa amemteua Mhandisi Peter Mwasalyanda kuwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasilinao kwa Wote ( UCSAF) kwa miaka mitano.
SOMA: Waziri Jerry Silaa akabidhiwa ofisi
Taarifa ya Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini imeeleza kuwa uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ya mwaka 2009.
SOMA: Waziri Slaa ateua bodi mpya
Aidha taarifa hiyo pia imeweka wazi kuwa uteuzi huo umeanza Oktoba 7, 2024 na kutamatika Oktoba 6 2029. Awali Mhandisi Mwasalyanda alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa UCSAF.
Comments are closed.