Simba hadi raha Tunisia

TUNISIA; BAO lililofungwa na Jean Ahoua limeiwezesha Simba ya Dar es Salaam kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunia mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi uliofanyika leo nchini Tunisia.

Kutokana na ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi 9 kwa michezo minne iliyocheza na kujijengea mazingira mazuri ya kufuzu Robo Fainali ya michuano hiyo.

Advertisement