Simba ilivyosonga mbele mabingwa Afrika

DAR ES SALAAM; SIMBA imesonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo kutoka sare ya bao 1-1 na Gaborone United katika mchezo wa marudiano wa michuano hiyo.
Kutokana na matokeo hayo Simba imefuzu kwa jumla ya mabao 2-1 kutokana na ushindi wa bao 1-0 iliyoupata mchezo wa kwanza baina ya timu hizo wiki iliyopita nchini Botswana.