Simba inaleta heshima kimataifa

DAR ES SALAAM; SIMBA inaleta heshima. Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa kwanza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), baada ya Simba leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Bao hilo pekee lilifungwa na kiungo Jean Ahoua kwa penalti baada ta beki mmoja wa Bravos kuunawa mpira wakati wa harakati za kuokoa.

Advertisement

Kipa Mousa Camara alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya Waangola, ikiwa ni pamoja na kudaka mkwaju wa penalti mwanzoni mwa kipindi cha pili.