Simba kuifuata Ahly leo

DAR ES SALAAM: MIAMBA ya soka nchini Simba leo jioni wataianza safari ya kwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya michuano ya African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly.
Taarifa iliyotolewa kupitia kurasa rasmi za mitandao za wababe hao Oktoba 21, 2023 imeeleza kuwa timu hiyo itaanza safari leo jioni.

Mchezo wa kwanza uliopigwa jana katika Uwanja wa Mkapa timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2.

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumanne, na ili Simba isonge mbele inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia mabao matatu ili kunufaika na kanuni ya goli la ugenini.

Habari Zifananazo

Back to top button