Simba SC wachangia damu, wananchi wahamasishwa

DAR ES SALAAM: Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kushirikiana na klabu ya Simba, imeanza rasmi zoezi la uchangiaji damu kuanzia jana na litaendelea hadi Septemba 10, 2025, kuelekea maadhimisho ya Simba Day.
 
Zoezi hilo linafanyika katika vituo vya damu salama vya kanda, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Wilaya pamoja na maeneo mbalimbali ya wazi.
 
Kampeni hiyo inalenga kuongeza akiba ya damu salama nchini na pia kuhamasisha mashabiki wa Simba pamoja na wananchi kwa ujumla kushiriki katika zoezi hilo kama sehemu ya maandalizi ya Simba Day, ambayo ni siku kubwa ya klabu hiyo.
 
Zoezi hili ni fursa ya pekee kwa mashabiki wa Simba kuonesha mshikamano na jamii kwa kuchangia damu na kuokoa maisha ya Watanzania.
 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button