BREAKING: Simba SC imeachana na kocha Robert Oliveira ‘Robertinho’ baada ya makubaliano ya pande zote mbili kwa maana ya klabu na mhusika.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia mitandao ya kijamii imeeleza kuwa pia wamefikia makubaliano ya kuachana kocha wa viungo Corneille Hategekimana.
Simba wameeleza katika kipindi hiki, timu itaongozwa na kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Suleiman Matola.