Simba yamnasa straika aliyecheza Kombe la Dunia

DAR ES SALAAM; SIMBA ya Dar es Salaam, mchana wa leo imetambulisha usajili wa mshambuliaji Mtanzania, Selemani Mwalimu kutoka timu ya Wydad AC ya nchini Morocco.

Nyota huyo raia wa Tanzania alikuwa sehemu ya kikosi cha Wydad kilichocheza michuano ya Kombe la Dunia la klabu iliyofanyika nchini Marekani Juni na Julai mwaka huu, na alicheza dakika 45 dhidi ya Juventus ya Italia na dakika 29 dhidi ya Al Ain ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button