Simba yazidiwa pointi saba na Yanga

BAADA ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC, Simba sasa imeachwa pointi saba dhidi ya Yanga anayeongoza msimamo wa Ligi Kuu akiwa na pointi 37, mtani wake akiwa na 30.

Mchezo huo unakamilisha idadi ya michezo 13 kwa Simba, ambapo inazidiwa mchezo mmoja dhidi ya Yanga.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Azam FC wenye pointi 32 ikiizidi Simba mchezo mmoja.

Katika mchezo wa leo, Azam ilianza kuandika bao la kuongoza lililofungwa na Price Dube dakika ya 14, kabla ya Clatous Chama kusawazisha dakika ya 90 kwa mkwaju wa faulo.

Habari Zifananazo

Back to top button