Sirro: Toeni ushahidi kesi za ukatili

KIGOMA: MKUU wa Mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro amewataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kutoa ushahidi wa kesi za matukio ya ukatili ili mahakama ziweze kutoa haki kwa watakaokutwa na hatia.

Balozi Sirro ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10, 2025 wilayani Kasulu mkoani Kigoma alipotembelea na kuzungumza na watendaji wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi wilayani humo.

Amesema uwepo wa vitendo vya ukatili katika jamii kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii yenyewe kushindwa kutoa ushahidi unaotosheleza kuwatia hatiani watuhumiwa.

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa chini ya Program ya Pamoja ya Kigoma (KJP) inayotekelezwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Balozi Sirro amesema kuwa athari ya jamii kutokuwa tayari kutoa ushahidi wa kesi za ukatili na badala yake mambo hayo kumalizwa kijamii kumesababisha matukio ya ukatili kuendelea mkoani humo.

Pamoja na changamoto hiyo, Sirro ameitaka jamii kudumisha malezi bora na yenye maadili kwa watoto hali itakayopunguza matukio ya ukatili Sambamba na kutoa wito kwa watendaji wa dawati hilo kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia utu na misingi ya sheria ili kulifanya dawati hilo kuwa kimbilio kwa wananchi wenye changamoto za vitendo vya ukatili.

Awali, Mkuu wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi wilayani Kasulu, Sperius Rweyemamu,amesema kuwa dawati hilo limesaidia kukabiliana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia wilayani humo ikiwemo vipigo, ubakaji na mulawiti ambavyo kipindi cha nyuma jamii ilikuwa inaaona kama jambo la kawaida.

Mratibu huyo wa dawati alitaja sababu zinazochangia kukwama kwa kesi za matukio ya ukatili wilayani humo kuwa ni pamoja na matukio kuamuliwa kwa ngazi ya jamii, uchelewaji wa kutoa taarifa zaidi ya saa 72 ya kisheria, wananchi kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi kwa kisingizio cha kukosa nauli na wakati mwingine ndugu wa waathirika kudai fedha kutoka kwa watuhumiwa.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button