DAR ES SALAAM; KAMPUNI ya Sixunited imezindua vishkwambi maalum ‘Acer e10 Series Notebook’ kwa ajili ya kuwarahisishia wafanyabiashara utendaji wao.
Uzinduzi wa bidhaa hiyo umefanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau pamoja na wafanyabiashara mbalimbali.
Meneja wa kampuni hiyo, hapa nchini Theresia Mwita amesema wamefanya hivyo ili kurahisisha upatikanaji wa teknolojia hiyo na kwamba hatua hiyo pia itasaidia kupatikana kwa ajira kwa vijana kupitia bidhaa hiyo itakayouzwa kwa gharama nafuu.
“Tumelenga kurahisisha upatikanaji wa teknolojia iliyo bora na kwa gharama nafuu, nitoe wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha hawakosi kifaa hiki, ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwao,”Alisema Theresia