ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameaziagiza taasisi zinazosimamia masoko mapya kuweka viwango vidogo vya malipo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili wamudu kulipa na kuendelea na biashara katika mazingira mazuri.
Rais Dk,Mwinyi alizungumza wakati alipofungua soko jipya la kisasa la Jumbi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk.Mwinyi amewahakikishia wafanyabiashara kuwa serikali itaendelea kuwaandalia mazingira bora zaidi yatakayoendana na soko hilo.
Rais Dk, Mwinyi amesisitiza kuwa serikali imetenga kiasi cha shillingi bilioni mia moja kwa ajili ya kuwapatia mitaji wajasiriamali na wafanyabiashara kuimarisha biashara zao .
SOMA: TRA kuwaongezea faida wafanyabiashara
Halikadhalika Rais Dk, Mwinyi ameruhusu wafanyabishara kufanya shughuli zao muda wote na kuagiza soko kuwa wazi Usiku na mchana.
Vilevile Rais Dk,Mwinyi amewaahidi wananchi kuwa ataendelea kujipambanua kwa Vitendo kutimiza ahadi alizoziahidi wakati wa Kampeni mwaka 2020.