Taasisi ya Mandela yasifiwa kwa tafiti bunifu

TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) imepongezwa na Wabunge wa Bunge Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kwa kufanya tafiti zinazolenga changamoto zinazozikumba jamii na viwanda Afrika.

Pongezi hizo zimetolewa Arusha mara baada ya wabunge wa EALA walipokwenda kutembelea taasisi hiyo chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Jumla ya Bunge hilo, Dk Abdullah Makame.

Makame amesema taasisi hiyo ni miongoni mwa taasisi zenye kuleta tija katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutokana na tafiti zao kulenda kutatua changamoto za kijamii pamoja na viwanda ambavyo huchochea ajira kwa wananchi

Amesema pia taasisi hizo imekijita zaidi katika gunduzi za aina mbalimbali pamoja na kuwezesha baadhi ya tafiti kuingia sokoni ikiwemo kuhakikisha changamoto za ajira zinatatulika kupitia kilimo au sekta za viwanda na nyinginezo.

Ambapo pia katika kikao cha pamoja Dk, Makame amepongeza mfumo wa elimu unaotolewa NM-AIST, ambao umejengwa juu ya nguzo tano kuu na kuongeza

Kwa upande wake, Naibu Makamu wa Taasisi anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ubunifu, Profesa, Anthony Mshandete alieleza kuwa tafiti zote zinazofanywa NM-AIST zimejikita katika kutatua matatizo halisi ya jamii.

Huku akisisitiza kuwa utafiti na ubunifu wa taasisi hiyo ni wa vitendo, unaolenga kuleta suluhisho endelevu kwa changamoto za kiafya, kijamii na kiuchumi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button