Taasisi yajizatiti mageuzi teknolojia

“Sekta ya teknolojia ni injini ya maendeleo. Tunazitaka kampuni na taasisi mbalimbali kuungana nasi katika kuendeleza juhudi za kulijenga taifa kiteknolojia kwa manufaa ya jamii na uchumi,”.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Dynatech Solutions Limited, Exaud Kimboi ametoa kauli hiyo katika mafunzo maalumu yanayolenga kuleta mageuzi katika teknolojia bunifu, hususan matumizi ya Akili Mnemba ili  kuchochea maendeleo ya sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Amesema kampuni yake imejipambanua kuwa sehemu ya suluhisho la mabadiliko ya teknolojia nchini kwa kutoa elimu inayohitajika ili kujenga mifumo ya kisasa na jengefu.

“Tumeandaa mafunzo haya ili kutoa uelewa mpana kuhusu teknolojia bunifu zitakazochochea ubunifu wa bidhaa madhubuti zenye matumizi mapana ya sayansi ya juu na Akili Mnemba,” amesema Kimboi.

Ameongeza kuwa teknolojia hizo zitasaidia kuboresha na kukuza sekta ya TEHAMA nchini kwa kuleta mabadiliko ya kimfumo na kimuundo yatakayowezesha uratibu bora wa shughuli za kila siku katika taasisi za fedha, elimu na teknolojia.

Kimboi pia amesisitiza juu ya ushirikiano wa karibu kati ya Dynatech na Serikali kupitia wizara na taasisi mbalimbali, akisema kuwa ushirikiano huo unaonesha namna kampuni hiyo imekuwa chachu muhimu ya mabadiliko ya kiteknolojia nchini.

Amefafanua kuwa Dynatech inaendelea kuwa mshirika mkuu katika kukuza mifumo ya TEHAMA, ikijikita zaidi katika usimamizi wa Cloud Database na uanzishaji wa mifumo mipya ya kisasa.

Kwa upande wake, Meneja wa Dynatech, Wangui Kaboreta, ameeleza umuhimu wa uwepo wa kampuni ya Oracle nchini, akibainisha kuwa kwa zaidi ya miaka 47, Oracle imekuwa ikitoa masuluhisho ya teknolojia kwa taasisi mbalimbali duniani.

Naye Gabriel Mwongera, Principal Senior Engineer wa Oracle, amewasilisha suluhisho jipya la Oracle linalotumia teknolojia ya Akili Mnemba ndani ya mifumo yake, hatua inayoongeza ufanisi katika utunzaji, uchakataji na usimamizi wa taarifa kwa taasisi za kisasa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button