Taasisi yamkumbuka Mwalimu Nyerere

DAR ES SALAAM: Kuelekea maadhimisho ya kumbukizi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, yanayoadhimishwa kitaifa kila Oktoba 14, Taasisi ya Amani Tanzania ‘Peace Solution Tanzania’ (PST) imetembelea nyumba ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Mariam Kihelelo, amewataka vijana nchini kuwa wazalendo na kujituma katika kulitumikia taifa, badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu.
“Vijana wengi siku hizi si wazalendo kama Baba wa Taifa alivyokuwa. Mwalimu Nyerere hakuwa mtu wa tamaa; aliishi maisha ya kawaida bila kujirundikia mali. Lakini vijana wa sasa wakipata ajira ndani ya mwaka mmoja wanataka wawe na kila kitu na kuishi maisha ya anasa,” alisema Bi. Kihelelo.
Kwa upande wake, Mhifadhi wa Mambo ya Kale katika Nyumba ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere, Emmanuel Katoroki, alisema mwaka huu wamepanga kutembelea taasisi, shule na wananchi mbalimbali ili kujua ni kwa namna gani wanamfahamu Baba wa Taifa.
Ametoa wito kwa wananchi kutembelea makumbusho hayo ili kujionea vifaa alivyotumia Mwalimu Nyerere, ikiwemo redio, pasi, cherehani na vyombo vya nyumbani, vinavyoonyesha maisha yake ya unyenyekevu na uzalendo.
Naye Mkurugenzi wa PST Mkoa wa Dar es Salaam, Gilbert Msowoya, ameisisitiza jamii kuendeleza amani, umoja na mshikamano aliouhimiza Mwalimu Nyerere, huku akitaka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuitumia kwa ujenzi wa Taifa, hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Oktoba 29.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa PST, Edward Mwaisonge, alisema amevutiwa na alama za uzalendo alizoziona ndani ya nyumba hiyo, ikiwemo sinia la chakula lililotumiwa na Mwalimu, linaloashiria umoja na usawa.
“Kupitia vitu hivyo, tumejifunza kuwa Mwalimu alithamini umoja na kutokuwa na matabaka. Ni somo kwa jamii yetu kuendelea kudumisha uzalendo ili taifa letu lisiwe rahisi kuvurugika,” alisema Mwaisonge.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com