MSEMAJI Wa Taasisi ya Dini ya Kiislam ya Twarika Kitengo Cha Idara Ya Habari, Shekhe Harun Hussein amewaomba wananchi wote nchini kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na kuwasihi wananchi ikiwemo viongozi wa dini kuhamasisha wananchi kujiandikisha.
Shekhe Harun ametoa rai hiyo Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuipongeza Tume ya Huru ya Uchaguzi kwa kutoa elimu kwa viongozi wa dini, mila, mashirika binafsi, asasi mbalimbali .
Amesema ni vyema wananchi kuhakikisha taarifa zao zinaingia katika daftari la mpigakura kwasababu ni muhimu ndani ya miaka mitano, hivyo viongozi wa dini,kimila, vyama vya siasa ni wajibu wao kutoa elimu hii ya uandikishaji ili wananchi wengi wajitokeze.
Ameomba NEC kufika hadi vijijini na kutoa elimu zaidi ya uandikishaji wapigakura katika daftari hilo la kudumu ikiwemo makundi maalum yashirikishwe kwakutengenezewa mfumo mzuri wa upataji elimu na uandikishaji katika daftari hilo.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuandikisha wapigakura wapya 224,499 sawa na ongezeko la asilimia 18 ya wapigakura 1,225584 waliopo kwenye daftari la wapigakura Mkoa wa Arusha.
Idadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kailima (INEC) Kailima Ramadhani wakati wa mkutano wa wadau wa Uchaguzi na Tume ya uchaguzi, ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Arusha.
Amesema baada ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga kura linalotarajiwa kufanyika kwa siku saba mkoani Arusha kuanzia Novemba 11 -17, 2024, mkoa wa Arusha utakuwa na jumla ya wapiga Kura 1,480,083.