Taasisi zapewa somo ziwajibike kwa jamii

DODOMA; Mwenza wa Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, Mama Neema Nchemba amehimiza aaasisi za umma na binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii kupitia utekelezaji wa programu za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Amesema hayo, Juni 16, 2026 katika hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali vilivyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika Hospitali ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya shirika hillo.

Ameishukuru, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya hususani ujenzi wa hospitali, utoaji wa ajira kwa wataalamu wa atya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zilizorahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini.

Amesema vifaa hivyo vilivyotolewa vinajumuisha vitimwendo 20, vitanda vya kujifungulia vitano, vitanda vya kufanyia uchunguzi vitano, vitanda vitano vya kulaza wagonjwa, machela moja ya kisasa, makabati matatu ya kuhifadhia vitaa tiba pamoja na mabeseni yenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya watu 30 waliojifungua.
Awali, akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Viwanda na Blashara, Judith Kapinga amesema Serikali itaendelea kuhimiza taasisi zake kutekeleza kwa vitendo sera ya uwajibikaji kwa jamii ili kuchangia kuboresha huduma za kijamii na maisha ya wananchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema mkoa wake uko tayari katika kushirikiana na wizara pamoja na TBS kwa ujumla katika kuendeleza sekta ya viwanda na biashara na jitihada za uwajibikaji kwa jamii katika mkoa wake.




78WIN ngày càng khẳng định sức hút với cộng đồng người chơi nhờ giao diện hiện đại, nhiều trò chơi chất lượng và trải nghiệm giải trí chuyên nghiệp trên mọi thiết bị. Một lựa chọn đáng chú ý cho anh em yêu thích cá cược và game trực tuyến 🎯
I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $35,000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by visiting Following Link…
.
You can check more……………… https://Www.Payathome9.Com