SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA) limeifungia klabu ya Tabora United kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji wa zamani wa timu hiyo Evariste Mutambayi Kayembe baada ya kushinda kesi yake dhidi ya klabu hiyo.
–
Taarifa iliyotolewa leo Novemba 7, 2023 na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imeeleza mchezaji huyo raia wa DR Congo alifungua kesi madai ya malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mshahara.
–
TFF imeeleza FIFA ilitoa siku 45 kwa Tabora United kumlipa mchezaji huyo hata hivyo haikutekeleza tangu hukumu hiyo ilipotolewa.
–
Wakati klabu hiyo ikijipanga kutekeleza adhabu hiyo, TFF pia imeifungia kufanya uhamisho wa wachezaji wa ndani.


4 comments