Takukuru Manyara yaonya ukipokea rushwa umekwisha

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imeonya hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya atakayebainika kutoa au kupokea rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Amesema kwa mujibu wa ibara ya (4) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na kwamba ibara ya (9) inasema moja kati ya jukumu kubwa la serikali ni kuondoa rushwa huku ibara ya (8) ikisema serikali itapata madaraka kutoka kwa wananchi na itawajibika kwa wananchi.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara, Bahati Haule amezungumza hayo leo wakati akitoa taarifa ya tathmini ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kuanzia Julai hadi September ambapo amesema lengo kuu ya ibara hiyo ni kuimarisha demokrasia na wananchi wajue kwamba wanatakiwa kutumia demokrasia hiyo kuharakisha maendeleo ya taifa.

“Tunakemea rushwa kwenye uchaguzi kwa sababu rushwa ni kosa la jinai, lakini pia rushwa ni kosa la kiimani, maandiko matakatifu kwenye vitabu vyote vya dini vinakataza rushwa, lakini pia ni kosa Kwa mujibu wa utumishi wa umma,ni kosaa kimaadili,kwaio rushwa ni adui wa haki na maendeleo,”

Aidha, Takukuru pia katika utendaji kazi wake imeweza kuokoa kiasi cha Sh milioni 13.8 ambapo kiasi Sh milioni 4.8 kilitokana na thamani ya dawa zilizoibiwa kwenye Zahanati ya Orkirung’rung na kurejeshwa baada ya kufanyika ufuatiliaji wa Takukuru.

Hata hivyo, mpango wa Takukuru Mkoa wa Manyara 2022/23 hadi 2025/26 itaimarisha juhudi za kuzuia vitendo vya rushwa kwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kuzuia rushwa kupitia nyezo mbalimbali za uelimishaji ikiwemo klabu za wapinga rushwa mashuleni na vyuoni.

Habari Zifananazo

Back to top button