WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi, Dk Pindi Chana amesema Serikali imekuwa ikitumia takwimu za kisayansi kufanya maamuzi yaliyojikita kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori ili kuwa na utalii endelevu.
Dk Chana ametoa kauli hiyo leo Oktoba Arusha alipozungumza na Menejimenti yaTaasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Njiro – Arusha ambapo amesema taasisi hiyo ni muhimu kwa uhifadhi nchini.
“Tunahakikisha rasilimali hii ya Wanyamapori ipo kwa kizazi cha leo na kijacho ambapo matumizi ya takwimu za kisayansi ni dira katika uhifadhi,” amesisitiza Waziri Chana.
Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dk Eblate Mjingo amesema takwimu za tafiti zinasaidia kunadi utalii ikiwa ni pamoja na kuelekeza namna bora ya kufanya utalii sambamba na kuimarisha uhifadhi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia utalii, Nkoba Mabula, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dk Thereza Mugobi, wawakilishi kutoka Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii na Maafisa Waandamizi kutoka TAWIRI.
Comments are closed.