Taliban yakana kushambulia msafara

PAKISTAN : KUNDI la wanamgambo wa Taliban la nchini Pakistan limekanusha kufanya shambulio la bomu dhidi ya msafara wa polisi uliokuwa ukiwasindikiza mabalozi wa nchi kadhaa katika eneo tete la kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.

Kauli hiyo ya msemaji wa kundi linalofahamika kama “Tehreek-e-Taliban-Pakistan” imetolewa wakati mamlaka za Pakistan zikisema bado zinaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini ni nani aliyehusika na shambulio hilo ambalo lilisababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi.

Mabalozi kutoka mataifa Indonesia, Ureno, Kazakhstan, Bosnia, Zimbabwe, Rwanda, Turkmenistan, Vietnam, Iran, Urusi na Tajikistan walishambuliwa hapo jana katika eneo la Malam Jabba wakiwa safarini kwenda Swat Valley, eneo ambalo liliwahi kuwa ngome imara ya kundi la Taliban nchini Pakistan.

SOMA :  Magaidi wauwa polisi 10 Pakistan

Habari Zifananazo

Back to top button