Taliban yakata mawasiliano

KABUL, Afghanistan: MAMLAKA ya Kiislam ya Taliban imeamuru kuzimwa kwa mkongo wa taifa wa intaneti nchini Afghanistan hadi pale itakapotoa tangazo jipya. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, hatua hiyo itakata huduma zote za mawasiliano ya kidijitali nchini humo na kuathiri mamilioni ya wananchi.
Tangu kurejea madarakani mwaka 2021, kundi la Taliban limekuwa likitekeleza masharti na vizuizi vikali chini ya sheria kali za Kiislamu, likidai vinahitajika kudhibiti uvunjifu wa maadili. SOMA:13 wafariki tetemeko Afghanistan