Tamisemi yaipa 5 TET

NAIBU  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI- Elimu, Dkt.Charles Msonde ameipongeza TET kwa kuweka maudhui ya elimu ya awali, MsingI, Sekondari na Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini katika mifumo wa kieletroniki, pamoja na kuweka vitabu vyote vya kiada katika Maktaba Mtandao.

Naibu Katibu Mkuu huyo ametoa pongezi hizo katika ziara yake ya siku moja aliyoifanya leo Desemba 18, 2022 katika ofisi za TET zilizopo jijini Dar es salaam.

Aidha, ameeleza kuwa ameguswa na kufurahishwa sana kwa TET kuweka vitabu vyote katika mfumo wa e-book jambo ambalo limerahisisha upatikanaji wa machapisho hayo na hivyo kurahisisha tendo al ufundishaji na ujifunzaji.

“Kwa kweli niwapongeze sana TET, hii ni hatua kubwa sana katika kuhakikisha upatikanaji wa vitabu kwa njia zote ikiwemo hii ya kupitia mifumo ya kieletroniki.”Amesema na kuongeza

“Kilichobaki kwetu TAMISEMI ni kuhakikisha uwepo wa vifaa vya TEHAMA vitakavyowezesha wanafunzi wote nchini kuingia katika mifumo hii na kujifunza.”Amesema Dkt.Msonde.

Dkt. Msonde katika ziara yake amepitishwa kwenye mifumo ya ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi na mfumo wa Maktaba Mtandao ya TET.

Pia alipata nafasi ya kutembelea studio za sauti na picha za TET pamoja na ghala la vitabu vya kiada vya kuanzia elimu ya Awali,Msingi na Sekondari lililopo EPZA ambako alielezwa namna kazi ya usambazaji na usafirishaji wa vitabu inavyofanyika.

Akiwa katika eneo la Maghala, Naibu Katibu Mkuu huyo ameipongeza TET kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuandaa vifaa saidizi vya kutekeleza mtaala kwa kutumia teknolojia na kuahidi kuwa atahakikisha kuwa halmashauri zote nchini zinatoa taarifa sahihi za takwimu za mahitaji ya vitabu yanayohitajika kwa wanafunzi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Msonde ameahidi ushirikiano kwa TET katika masuala yote hususani kwenye suala la mafunzo kazini kwa walimu na kwenye matumizi ya Maktaba Mtandao ambapo atawahamasisha viongozi na walimu wote katika Halmashauri kushiriki katika mafunzo na kutumia Maktaba Mtandao hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET-Dkt. Aneth Komba amemshukuru Naibu Katiku Mkuu huyo kwa kutenga muda wa kuitembelea TET na kusema kuwa wataendelea kutekeleza kwa vitendo juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kuboresha elimu kwa kuhakikisha kuwa majukumu yote ya TET yanatekelezwa kwa ufanisi hususani kuhakikisha kuwa utoaji wa mafunzo kwa walimu kazini unafanyika ipasavyo na kuwa vifaa vya Kiada vya kujifunzia na kufundishia vinaandaliwa kwa ubora na vinapatikana kwa wakati katika nakala ngumu na kwa kutumia mifumo mbalimbali ya kiteknolojia.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Lucy Mgila
9 months ago

Mungu awe tayari pamoja nasi.
Amen.

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x