Tamisemi yaunga mkono bunifu za Temdo

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Adolf Ndunguru amesema TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) kwa kuzihamasisha halmashauri zote nchini kutumia bidhaa na vifaa tiba vinavyozalishwa na shirika hilo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan kwenye sekta za afya, elimu na kilimo.

‎Ameyasema hayo jijini Arusha alipotembelea taasisi hiyo na kujionea jinsi bidhaa hizo zinavyozalishwa na jinsi taasisi zilizo chini ya TAMISEMI zinavyoweza kushirikiana na TEMDO katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na ya kimkakati.

Amebainisha kuwa katika kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, Serikali itaendelea kuhakikisha sekta ya afya inaimarika ukiwa ni pamoja na kutumia vifaa tiba bora imara vinavyopatikana kwa gharama nafuu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk, Hashil Abdallah ameihakikishia TAMISEMI kuwa TEMDO ina uwezo wa kutengeneza vifaa tiba kwa viwango vya kimataifa vilivyothibitishwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) pamoja na Bohari ya Dawa (MSD) na kuwa iko tayari kutoka huduma kwa Halmashauri zote nchini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button