Tamthilia ya ‘Bunji’ yatabiriwa kuleta mapinduzi

DAR ES SALAAM: Tamthilia ya Bunji imetabiriwa kuleta mabadiliko makubwa katika kiwanda caha uigizaji nchini kutokana na uwekezaji uliofanyika.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa Tamthilia hiyo jijini Dar es Salaam, Msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza amesema kuwa uzalishaji wa tamthia hiyo umezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji wa kisasa na ubora wa hali ya juu.

“Tunaendelea kuisukuma sanaa kitaifa na kimataifa na ukanda wote hasa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara” amesema Mgaza.

Amesema, tamthilia hiyo itaonyeshwa kwa mara ya kwanza 1 Aprili mwaka huu.

Aidha, Mgaza amesema tamthilia ya ‘Bunji’ inamuhusisha kijana mmoja ambaye ni mhitimu wa udaktari na ni Daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi, lakini ndoto yake ni kuwa mpiganaji wa kulipwa.

Akiendelea kuelezea Tamthilia hiyo, Mgaza amesema baada ya kuhitimu, analazimika kufanya kazi katika hospitali ya familia na siku ya kwanza anagundua kuwa familia yake inafanya biashara haramu kupitia mgongo wa hospitali.

“Miongoni mwa waigizaji mashuhuri katika tamthiliya hii ni pamoja na Isarito Mwakalindile, Twaha Kiduku, Nyota Waziri, Dk. Nnyaka Godwin, Carpoza Edward, Fatma Hassan n.k”

Kwa upande wake mwigizaji wa tamthilia hiyo, Isarito Mwakalindile ameishukuru timu yake yote iliyohakikisha tamthiliya inafika mbali na changamoto walizokutana nazo wakati wakiandaa.

Habari Zifananazo

Back to top button