TANAPA yaguswa na upungufu wa damu hospitalini

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeeleza kuguswa na changamoto ya upungufu wa damu kwenye hospitali nchini na kuahidi kupitia maofisa na askari wake kuwa mchangiaji wa kudumu wa damu salama.

Ofisa Uhusiano wa TANAPA, Christine Mbena amesema hayo baada ya maofisa wa TANAPA Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo kuchangia Damu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH).

Mbena amesema hatua hiyo inakuja kwa kuzingatia kuwa maofisa na askari wa TANAPA ni sehemu ya jamii na hivyo wanajiona kuwa wana wajibu wa kuchangia damu kila wakati ili kuokoa maisha ya watanzania.

SOMA: ‘Watanzania changieni damu uhitaji ni mkubwa’

Amesema mbali na kusaidia kuongeza akiba ya damu salama kwenye hospitali lakini pia mpango huo unalenga kuongeza ushirikiano kati ya jamii na TANAPA katika shughuli za uhifadhi wa maeneo ya maliasili.

“Tumezoeleka kuwa mara nyingi tunakuwa maeneo ya uhifadhi kwa kuwa ni askari, ni walinzi wa maliasili pia ni wananchi wa Tanzania na ni wanajamii lakini ni binadamu ambao tuna uhai”, amesema.

Naye Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Dk Imani Kikoti amesema jumla ya maofisa wa TANAPA 31 wameshiriki uchangiaji damu katika hospitali ya CZRH na zoezi limefanyika kwa hiari.

“Tumewiwa kuchangia damu katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Chato kwakuwa hii ni hospitali inayohudumia jamii inayotuzunguka, lakini pia na wateja wetu kutoka maeneo mbalimbali.”, amesema.

Msimamizi wa Huduma za Maabara CZRH, Dk Awadhi Mujuni amesema mahitaji ya damu hospitalini hapo ni makubwa ambapo kwa siku ni uniti 10 sawa na wastani wa uniti 300 kwa mwezi.

Dkt Mujuni ametaja makundi yanayohitaji zaidi damu salama ni waathirika wa ajali za barabarani, wanawake wanaotoka kujifungua na watoto wenye magonjwa ya seli mundu.

Aidha amewashukuru TANAPA kwa mchango wao na kuziomba taasisi nyingine kushiriki uchangiaji damu hospitalini hapo kwani ina uwezo kwa kuhifadhi damu kuanzia uniti 1,000.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hosptali ya CZRH, Dk Brian Mawala amewahakikishia watanzania kuwa hospitali ya kanda Chato imejizatiti kuokoa maisha ya watu kupitia uwepo wa huduma ya damu salama ya uhakika.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button