TANAPA yajizatiti kuongeza mazalia ya samaki Ziwa Victoria

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeweka mpango maalum kufanikisha ongezeko la mazalia ya samaki ndani ya Ziwa Victoria kiwango ambacho kimetajwa kushuka siku hadi siku kutokana na uvuvi haramu.

TANAPA inatekeleza mpango huo kwa kuongeza uwekezaji katika ulinzi wa maeneo ya hifadhi ya mazalia ya samaki na utoaji wa elimu kwa wakazi wanaozunguka mwambao wa Ziwa Victoria kulinda mazalia hayo.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi, Dk Imani Kikoti ameeleza hayo katika ziara maalum ya waandishi habari mkoani Geita katika hifadhi hiyo.

Kikoti amesema katika kutekeleza mpango huo, hifadhi ya kisiwa cha Rubondo inahakikisha mazalia ya samaki yanakuwa salama na imetenga eneo la mazalia ya samaki katika fukwe zenye urefu wa Km 150.

“Mpaka sasa hivi sekta ya uvuvi ndani ya Ziwa Victoria imeendelea kushuka, kwa maana kwamba maeneo mengi wavuvi hawapati mazao ya samaki ya kutosha tofauti ilivyokuwa hapo kipindi cha nyuma.

“Tumejitahidi sana kuhakikisha kwamba mazalia ya samaki yanakuwa salama, na yakishakuwa salama tunatarajia kwamba yatasaidia kuongeza uzalianaji wa samaki ili kuongeza idadi ya samaki,” amesema.

Ameeleza tathimini ya awali inaonyesha kuwa Ziwa Victoria linahudumia zaidi ya watu milioni 4.5 ambapo juhudi za haraka zinahitajika kunusuru mazalia ya samaki ambapo elimu ya ufugaji wa samaki inatolewa.

Ofisa Uhifadhi Mkuu Kitengo cha Ulinzi Kisiwa cha Rubondo, Agricola Roman.

Ofisa Uhifadhi Mkuu Kitengo cha Ulinzi Kisiwa cha Rubondo, Agricola Roman amesema TANAPA imeimarisha ulinzi na usalama kwa ajili ya doria za mara kwa mara kwenye maeneo ya mazalia ya samaki.

Agricola amesema mbali na ulinzi wa mazalia ya samaki bado kuna changamoto kubwa ya uvuvi usiozingatia taratibu nje ya maeneo ya hifadhi hali inayorudisha nyuma juhudi zinazofanywa kuongeza idadi ya samaki.

“Sheria za uhifadhi zinakataza kuingia kwenye maeneo ya hifadhi bila kibali lakini bado kuna majangili wanaingia na wengine wanatumia nyavu haramu jambo ambalo ni hatari kwa mazalia ya samaki”, amesema.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am making a real GOOD MONEY (80$ to 92$ / hr. )online from my laptop. Last month I GOT a check of nearly 21,000$, this online work is simple and straightforward, I don’t have to go to the OFFICE. At that point this work opportunity is for you. If you are interested. Simply give it a shot on the accompanying site link… https://Www.EarnApp1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button