Tanesco yapewa siku 7 kufikisha umeme bweni la Shishiyu

SIMIYU: KATIBU wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi ametoa siku saba kwa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha umeme umefika katika bweni ya wasichana katika Shule ya Sekondari Shishiyu wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Kihongosi ametoa agizo hilo alipofika katika shule hiyo na kukagua bweni hilo mkoani himo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza baada ya kukagua bweni hilo Kihongosi alisema kama chama wameridhishw ana kufurahishawa na kazi kubwa iliyofanywa kwa ajili ya watoto wa shile hiyo lakini kazi hiyo haiwezi kuwa na tija kama pataendelea kukaa bila umeme.

“Sasa nitoe tu jambo moja hapa nimeambiwa katika bweni hili umeme haupo Meneja wa Tanesco nikupe muda gani umeme waki hapa, wiki moja ni siku saba umeme uwake na tutafuatilia Mwenyekiti wa mkoa fuatilia hapa waleti umeme,” alisema kihongosi.

Alisema wafanya hivyo ili watoto hao watakaporudi shule wakute miundombinu yote imekaa vizuri, akieleza kuw awatoto hao watafarijika na kufurahi wakiwa katika bweni hilo.

Akisisitiza watu wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kutembea katika maeneo mbalimbali ya nchi ya nchi kuona mageuzi na maendeleo yaliyofanyika, badala ya kukaa mijini na kusema kuwa hakuna maendeleo ambayo yamefanyika katika maeneo mengine.

Kwa mujibu wa ujenzi huo umegharimu jumla ya Sh milioni 160 ambazo walifadhiliwa na OPEC kwa kupitia miradi ya kaya masikini TASAF awamu ya tatu ambazo zilitolewa katika shule za sekondari shilingi mbili ya magweni matano ya kujengwa miradi ya kupitia ufafili.

Pia vijiji hivyo vilichangia nguvu kazi, uchanga, mawe, kokoto, kusomba maji, kutimba misingi na usimamizi wa jumbe wa kamati mbili za kijamii (CMC) kwa vijiji viwili na mradi huo ulijengwa chini ya mkataba namba 24494 na ulianza kutekelezwa Oktoba 30,2025.

Mradi huo ulilenga hasa kuboresha mazingira ya masomo kwa watoto, hususani wa kike waliokuwa wakitembea umbali mrefu kila siku kwenda na kurudi shuleni ambao unatarajiwa kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na kupunguza au kuondoa mimba zisizotarajiwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button