Tani 18 dawa za kulevya zadakwa Dar

DAR ES SALAAM :MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imekamata shehena ya dawa mpya ya kulevya aina ya mitragyna speciosa mifuko 756 yenye uzito wa jumla ya kilogramu 18,485.6 sawa na tani 18.5 iliyokuwa ikiingizwa nchini kama mbolea.

Hayo yamesemwa leo na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, katika tukio hilo watuhumiwa saba wamekamatwa, wakiwemo raia wawili wa nchi ya Sri – Lanka ambao ni Jagath Prasanna Madduma Wellalage (46) na Santhush Ruminda Hewage (25).

“Watanzania waliokamatwa ni Riziki Abdallah Shawej (40), Andrew Athanas Nyembe (34), Mariam Shaban Mgatila (40), Ramadhan Sanze Said (57) na Godwin Melchory Maffikiri (40).

“Dawa hizi zilikuwa kwenye kontena lenye ukubwa wa futi 40, zikitokea nchini Sri -Lanka.”

Amesema Hiyo ni mara ya pili kukamatwa kwa aina hii ya dawa mpya ya kulevya, ambapo mwezi Juni mwaka huu, walikamata mifuko 450 yenye zaidi ya uzito wa tani 11.5 za dawa hizo zilizoingizwa nchini kama mbolea ikiwa kwenye kontena lenye ukubwa wa futi 20 ikitokea nchini Sri – Lanka.

” Hivyo, kufanya jumla ya kilogramu 30,082.03 sawa na tani 30 za dawa hizo kukamatwa kwa kipindi kifupi hapa nchini,” amesema.

Amesema kuwa, Mitragyna Speciosa ni dawa mpya ya kulevya (New psychtropic Substance-NPS) inayotokana na mmea unaofahamika kwa jina la Kratom ambao hupatikana zaidi katika nchi za Kusini Mashariki mwa Bara la Asia.

Amesema,dawa hiyo ya kulevya ina madhara sawa na dawa za kulevya jamii ya Afyuni (Heroin, Morphine).

“Dawa hii huathiri mfumo wa fahamu pamoja na kusababisha uraibu na vifo vya ghafla. Kutokana na kuongezeka matumizi ya dawa ya Mitragym Speciosa duniani, pamoja na madhara yanayosababishwa na sumu zilizomo katika dawa hii, nchi nyingi duniani zimezuia uzalishaji, usafirishaji na matumizi yake,” amesema.

Amesema kuwa, ukamataji wa Mitragyna Speciosa ni ishara ya kuwepo kwa changamoto mpya katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I am making a good s­al­ary from home $4580-$5240/week , which is amazing und­er a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now its my duty to pay it forward and share it with Everyone,

    Here is I started_______ http://Www.EarnApp1.Com

  2. I am making a good s­al­ary from home $4580-$5240/week , which is amazing und­er a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now its my duty to pay it forward and share it with Everyone,

    Here is I started_______http://www.join..money63.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button