TANROADS Tabora yarejesha mawasiliano Bukumbi – Kahama

TABORA: WAKALA wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Tabora, imerejesha mawasiliano ya Barabara ya Bukumbi kuelekea Kahama ambayo ilikatika kutokana na gari la mizigo kuzidisha uzito.

Kutokana na mzigo huo kuwa mzito gari hilo lilipasua karavati ambalo lilisababisha maji ya mvua kusambaa kwenye eneo lenye urefu wa Kilometa 1.2 kati ya hizo mita 800 zipo upande wa Tabora na mita 400 upande wa Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa leo Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora Raphael Mlimaji amesema eneo la barabara lililokatika ni Kati ya Kijiji cha Muhulidede Kata ya Ishihimulwa, Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora Kilomita 108 kufika Tabora mjini na Kijiji cha Busule kata ya chona, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

 

Amesema Desemba 14, 2023, saa tisa usiku gari la mizigo aina ya fuso lililokuwa limebeba shehena ya Karanga lilipita katika barabara hiyo inayounganisha Mkoa wa Tabora na Shinyanga kupitia Wilaya za Uyui na Kahama.

Amesema kutokana na kuzidisha uzito na siku hiyo mvua kubwa zilinyesha gari hiyo ilipasua Kalvati zilizojengwa zamani kwenye barabara hiyo ambayo awali ilikuwa ni ya Halmashauri na baadae kuletwa TANROADS ili ifunguliwe iwe inapitika na Wananchi.

 

Amesema kufuatia athari hiyo TANROADS imeamua kukata maeneo manne tofauti na kupanga mawe ili kuwezesha maji yatakayokuwa yameongezeka kupita chini wakati vyombo vya moto na watu wakipita juu ya barabara pasipo kusimama kwa huduma za usafiri na usafirishaji.

Ameeleza kuwa barabara hiyo inapitisha shehena nyingi zinazotoka Mikoa mbambali ikiwemo Katavi, Mbeya na maeneo ya Jirani kutokana na uwepo wa Maghala mengi ya chakula Kahama ambayo yanahudumia Nchi za Burundi, Rwanda na Kenya.

 

Raphael alieleza kuwa kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali kwa sasa barabara hiyo inapitika kwa asilimia 100 na kwamba kutokana na ufupi wa barabara hiyo magari mengi yamekuwa yakipita katika barabara hiyo hasa nyakati za usiku kwa sababu wanaona wakipita mchana wanaweza wakashtukizwa kwa kuwekewa mizani ya mkeka kwa jili ya kupima uzito.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button