Tanzania ijipange sawasawa neema ya urani

JUZI Rais Samia Suluhu Hassan alizindua ujenzi wa kiwanda cha majaribio cha uchenjuaji wa madini ya urani katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Uzinduzi wa kiwanda hicho kinachojengwa na Kampuni ya Mantra unaifanya Tanzania kutarajia kupata manufaa makubwa katika mradi wa uchenjuaji madini ya urani nchini.
Manufaa hayo ni pamoja na uwekezaji wa Dola za Marekani bilioni 1.2 huku serikali ikiingiza mapato ya Dola za Marekani milioni 40 kwa mwaka.
Kwenye uzinduzi huo, Rais Samia alieleza faida za uwekezaji huo wenye mapinduzi makubwa ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa ajira takribani 4,000 wakati wa ujenzi wa miundombinu 750 za kudumu.
Faida hizi na nyingine nyingi kwa mujibu wa Rais Samia zitapatikana kwa zaidi ya miaka 20 ya uchimbaji wa madini hayo nchini.
Kwanza tunaipongeza Serikali ya Rais Samia kwa namna inavyotekeleza ajenda za kitaifa zinazoleta mapinduzi makubwa ya uchumi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayotaka Tanzania kuwa taifa lenye viwanda na kufikia uchumi wa kati ngazi ya juu unaojitegemea ifikapo mwaka 2050.
Tunaipongeza serikali kutokana na ukweli kwamba, Dola za Marekani bilioni 1.2 zitakazowekezwa kwenye mradi huu na ajira zitakazopatikana zitawanufaisha kwanza Watanzania ambayo ndio dhamira ya dhati ya serikali kutekeleza mradi huu.
Kuzinduliwa kwa mradi huu wa kihistoria uliosubiriwa kwa miaka mingi unaashiria ushindi na uhuru wa kiuchumi kwa taifa hivyo ili kupata mafanikio hayo na mengine ambayo hayajaainishwa kwa sasa, watendaji wa serikali, wanasiasa na wananchi wanapaswa kujipanga sawasawa kufikia malengo hayo.
Mafanikio hayo hayaitegemei serikali peke yake bali kama alivyosema Rais Samia inahitajika nguvu ya pamoja ambayo pia imetafutwa muda mrefu kutafuta njia sahihi, salama na zenye manufaa kwa taifa kutumia rasilimali Tanzania ilizojaliwa na Mungu hususani madini haya ya urani ambayo huzalisha nishati ya nyuklia na tiba ya saratani.
Kwa mujibu wa taarifa za kitaalamu, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Afrika zilizobarikiwa madini haya na eneo la Mto Mkuju yatakapochimbwa madini hayo, kuna uwezo wa kuzalisha tani 300,000 kwa mwaka.
Tunaamini kupitia uwekezaji huu, Tanzania inajiweka katika nafasi ya kuwa kitovu cha utafiti na uchakataji wa urani kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati hasa kwa kuwa takwimu zinaonesha Afrika inadaiwa kuwa na asilimia 20 ya madini haya lakini ni asilimia kidogo imechakatwa.
Tunaungana na serikali kuhimiza kila sekta ya kimkakati ijipange kwa hili zikiwamo taasisi zinazosimamia utunzaji wa mazingira ili kuepuka athari zozote zinazoweza kuhatarisha utekelezaji wa mradi huu.
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do……. https://Www.Workapp1.Com
I have not checked in here for a while as I thought it was getting boring, but the last several posts are great quality so I guess I’ll add you back to my everyday bloglist. You deserve it my friend 🙂