DAR-ES-SALAAM: TUZO za Kimataifa zinazojulikana kama Hap Awards zinatarajia kufanyika nchini Tanzania katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Agosti 10, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kedmon Mapana amesema kuwa tuzo hizi zimegawanywa kwenye vipengele vikuu vitatu.
“Kutakuwa na vipengele vya Muziki, Mitindo na Filamu ambapo tuzo hizo zitatolewa katika usiku huo, kipengele cha muziki watashindanishwa wasanii wa muziki wa Dansi, Singeli Taarabu pamoja na ngoma za asili”, amesema
Aliongezea kuwa “Majaji watakuwepo kutoka nchini Marekani na wengine kutoka hapa nchini Tanzania ambao watakuwa wakifanya mchujo katika vipengele hivyo hadi kutapa mshindi, kutakuwa na Vipengele vya Muziki 11, 21 Fashioni pamoja na vipengele Filamu 11.”amesema Mapana.
SOMA: Burna Boy Ashinda Tuzo ya Msanii bora Afrika MEMA 2022
Kwa upande wake Mrisho Mrisho ametangaza vipengele Muziki wa Bongo fleva, huku mitinda wakichuana Asia Idorus pamoja na Mustaph Hasanal.
“Bongo fleva Tanzania watawania wasanii chipukizi watakuwa Yammi Vannillah Founder TzMrs Energy Aslam TZ, Best artist (Muziki wa dansi) Malaika Band, Twanga Pepeta, Msondo Ngoma, Mlimani Park, Orchestra, Mjengoni Band,” alisema Mrisho