Tanzania kudhibiti Mpox

DAR-ES-SALAAM : WIZARA ya Afya imeanza kuchukua hatua ya kuwachunguza wasafiri wanaoingia na kutoka ikiwa ni sehemu ya hatua ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya nyani, ambao ulitangazwa na Shirika la Afya Duniani WHO kuwa dharura ya kiafya.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afya kwa Umma, Dk Norman Jonas amesema ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya homa ya nyani nchini tayari wizara ya Afya imeanza kuchukua hatua ya kuwachunguza wasafiri.

Dk Norman amesema, kwa kuwa Tanzania ina mwingiliano na nchi ambazo tayari zinamaambukizi ikiwemo DR Congo, Burundi na Kenya, tayari ufuatiliaji wa wasafiri na wakazi unaendelea kufanyika na kuendelea kutoa elimu ya kujikinga kwa wananchi.

Tanzania imekuwa na muingiliano wa karibu na taifa jirani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani – WHO, karibu watu 15,000 wamegundulika kuambukizwa virusi vya mpox nchini humo katika mwaka wa 2024, huku kukiwa na vifo 500.

SOMA: Dola milioni 18.5 kudhibiti Mpox

 

Habari Zifananazo

Back to top button