Tanzania kunufaika soko la pamoja Afrika

DAR ES SALAAM: Serikali ya Tanzania itaendelea kunufaika na soko la pamoja la Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) na kuchagiza utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2050.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo wakati wa Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) uliofanyika Juni 30,2026 Jijini Abuja, Nigeria.

Londo amesema Soko huru la Afrika lina zaidi ya watu bilioni 1.4 ambapo ni idadi kubwa na inafanya kuwa ni soko la uhakika hivyo kuendana na utekelezaji wa mkakati wa Dira ya Maendeleo 2050 ya kuwa na uchumi wa Viwanda na kuongeza thamani ya bidhaa.

Aidha Londo amesema kuwa uwepo wa Jumuiya hiyo na Mikutano kama hiyo ina maslahi mapana kwa nchi ya Tanzania kwani inachagiza jitihada na ndoto za nchi za kufikia uchumi wa viwanda na kuwa na uhakika na soko.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button