Tanzania, taasisi Uswis kushirikiana kutokomeza magojwa

GENEVA: Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Global Fund zitaendelea kushirikiana katika vipaumbele vya Serikali vinavyolenga kutokomeza magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo Mei 30, 2024 kwenye kikao na Mkuu wa Usimamizi wa Ruzuku wa Global Fund, Mark Eldon-Edington kilichofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 77 wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Geneva nchini Uswisi.

“Nakushukuru sana Bw. Eldon-Edington kwa kuwa Taasisi yako ya Global Fund imechangia kwa kiasi kukubwa nchini Tanzania kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria na pia kuimarisha mifumo ya afya iliyo stahimilivu na endelev,” amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema kwa sasa changamoto kubwa iliyopo katika sekta ya afya ni kutomudu ugharimiaji wa baadhi ya vipaumbele vya kukabiliana na magonjwa pamoja ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaleta athari kubwa katika kutoa huduma za afya.

Kwa upande wake Eldon-Edington ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika kupunguza maambukizi mapya na vifo vitokanavyo na Ukimwi.

“Global Fund itaendelea kutoa kipaumbele kwa Tanzania katika kutoa msaada ili kuimarisha mifumo ya afya itakayowezesha uendelevu katika mwitikio wa kutokomeza magonjwa haya,” amesema Eldon-Edingtona

Habari Zifananazo

Back to top button