Tanzania yaongoza utawala fedha za umma

DODOMA: MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania   (NBAA), CPA Pius Maneno, amesema Tanzania inaongoza katika masuala ya utawala wa fedha za umma.

Akizungumza katika  ufunguzi wa semina ya siku tano kwa wakaguzi wa serikali jijini Dodoma, CPA Pius amebainisha kuwa masuala ya ukaguzi wa fedha, utoaji wa taarifa za fedha kwa uadilifu na matumizi ya viwango vipya  utaweza  kusaidia kuendeleza uchumi wa nchi.

“Hii ni taaluma pekee duniani inayofanya kazi kwa niaba ya maslahi ya umma,” amesema CPA Puis

Kwa upande wake, Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Isaya Jeremiah, amesema ni muhimu kwa watumishi kupewa mafunzi ya kimataifa ili kuboresha utendaji kazi .

Nae Shamimu Mshana, ameeleza furaha yake kushiriki mafunzo hayo, akisema kuwa yamekuwa na msaada mkubwa hasa wakati huu wa ukaguzi wa fedha za umma.

SOMA: Washiriki mafunzo NBAA watakiwa kuboresha ufanisi

“Mafunzo haya yanatupa maarifa mapya na yanatusaidia kumwezesha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoa ripoti zenye viwango vya juu,” amesema Shamimu

Habari Zifananazo

Back to top button