Tanzania Yashiriki Maadhimisho ya Jamhuri

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imeungana na Jamhuri ya Kenya katika maadhimisho ya Siku ya Jamhuri (Jamhuri Day) yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi.
Katika maadhimisho hayo, Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi (Mb), ambaye amemuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Tanzania na Kenya zina uhusiano wa muda mrefu wa kidugu na kihistoria, uhusiano ambao umeendelea kuimarika siku hadi siku. Mataifa haya mawili hushirikiana katika masuala ya diplomasia, uchumi, siasa, usalama, utamaduni na kijamii, pamoja na majukwaa ya kikanda na kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN). SOMA: Baraza la Mawaziri (SCTIFI) wakutana Kenya




