Tanzania yasisitiza ukuta wa kijani

NAIBU wa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis akishiriki Mkutano wa 16 wa Mkataba wa Kupambana na kuenea kwa Jangwa unaofanyika Saudi Arabia amhapo alitoa msimamo wa nchi kuendelea na jitihada za kuhifadhi na kutunza mazingira hususan kuweka msisitizo katika jitihada ya kuwa na ukuta wa kijani kwa kupanda miti. Katika Ujumbe wa Tanzania Naibu Waziri Khamis ameambatana na Naibu katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Hassan Mitawi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Agnes Meena na wataalamu.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)