TARURA Ruvuma kutekeleza miradi ya bil 22/-
WAKALA ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Ruvuma umeendelea kunufaika na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika miundombinu ya barabara, hatua inayochochea maendeleo ya kiuchumi, kilimo, na uhifadhi wa mazingira.
Meneja wa TARURA mkoa huo, Mhandisi Silvester Chinengo, amesema kwa mwaka wa fedha 2025/2026, mkoa unatekeleza miradi ya maendeleo yenye bajeti ya shilingi bilioni 22, ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka bilioni 7 za awali.
“Kwa sasa, TARURA Ruvuma inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 7,147, ambapo kilomita 133.69 ni za lami, 1,651.8 ni za changarawe, na 5,360.6 ni za udongo. Takribani asilimia 70 ya barabara hizo zinapitika msimu wote, jambo ambalo limeleta mabadiliko chanya kwa wakulima na wafanyabiashara wa mkoa huo,”amesema.
SOMA: Wakandarasi wa TARURA watakiwa kutekeleza miradi kwa ufanisi
“Barabara hizi zimekuwa mkombozi kwa wakulima. Mazao kama mahindi na kahawa sasa yanafika sokoni kwa wakati, bila kuharibika njiani na hivyo kuongeza uchumi kwa wakulima”, amesema Mhandisi Chinengo.
Aidha, Meneja huyo amesema TARURA imefanya manunuzi ya mikataba 43 yenye thamani ya sh bilioni 12.1, na iko katika hatua za mwisho za kusaini mikataba hiyo.
Ameongeza kusema kwamba kwa mwaka uliopita pekee, zaidi ya kilomita 3 za barabara za lami zimejengwa, na taa za barabarani zimewekwa ili kuongeza usalama na mwonekano wa mji kwa usiku.
“Kwa sasa, kila barabara inayojengwa inaambatana na uwekaji wa taa hatua inayoongeza usalama na kuchochea shughuli za kiuchumi hasa nyakati za usiku.”
Katika kulinda mazingira, Mhandisi Chinengo amewataka wananchi kutotupa taka kwenye mitaro ya maji na kushiriki katika utunzaji wa miundombinu.
“Serikali imewekeza fedha nyingi ni jukumu letu kuhakikisha barabara hizi zinadumu kwa muda mrefu kwa kuepuka uharibifu wa makusudi,” amesisitiza.
Naye, mkazi wa Makambi, Eva Ndomba amesema awali barabara zilikuwa na nyasi, vumbi na hata pikipiki zilikuwa zinapata changamoto kupita ila wanaishukuru Serikali kwa ujenzi wa barabara za lami kwani wanapita vizuri na uwekaji wa taa umewasaidia kwa sasa wanafanya biashara hata usiku.




Freedom to work whenever I want — that’s what I love! I made $18,542 in a month doing this online. Check the details ———————⊃⫸ https://dailycash21.blogspot.com/