‘Tathmini yaonesha utekelezaji wa lishe umepiga hatua nzuri’

SERIKALI imesema tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa mwaka 2024/2025 imeonesha kupiga hatua nzuri ya utekelezaji. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Profesa Shemdoe amesema Tanzania imeendelea kupiga hatua kuboresha hali ya lishe na hivyo kuimarisha nguvukazi ya taifa lenye afya bora inayochangia kikamilifu ukuaji wa uchumi. Takwimu zinaonesha Tanzania imepiga hatua ya utekelezaji wa masuala ya lishe kwa asilimia 99.9.
Pia, zinaonesha asilimia 30 ya Watanzania wana uzito uliozidi, huku na asilimia 10 wakiwa na unene uliokithiri. Profesa Shemdoe amesema uwekezaji katika lishe ya watu ni mkakati wa kiuchumi wenye tija kubwa na kwa kutambua umuhimu huo, Dira ya Maendeleo 2050 imeweka kipaumbele cha kujenga jamii yenye afya, ikitilia mkazo suala la lishe ili kuwa na jamii ambayo kila mtu anastawi kutokana na lishe bora.
Amesema pia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025/2030 inatambua umuhimu wa lishe katika kujenga na kulinda afya za wananchi, hivyo serikali ya CCM itahimiza na kusimamia upatikanaji wa lishe bora kwa wote. Profesa Shemdoe alisema lishe bora ni ulaji unaofaa wa vyakula vyenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ambao unatoa matokeo ya kutokuwepo kwa magonjwa kwa binadamu.
Amesema kwa sasa Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuanza utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ili kutoa matibabu stahiki kwa watu wote na kumshinda adui maradhi. Taasisi zapewa miezi 3 usajili kulinda taarifa binafsi Mamlaka. SOMA: Jamii yakumbushwa kuzingatia lishe bora



