TCCIA, EABC kutoa mitaji kwa vijana nchini

CHEMBA ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na East Africa Busuness Consortium(EABC) wamesaini mkataba wa makubaliano ya kuwawezesha vijana mitaji na elimu ya ujasiriamali ikiwa ni hatua ya kuwawezesha vijana kujiajiri.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini Mkataba huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa EABC, Imani Kajula amesema makubaliano hayo yanalenga kutumia taasisi zote mbili kuleta maendeleo makubwa katika kukuza ujasiriamali nchini.

“Wote tunajua ajira sasa ni changamoto na asilimia 80 ya watanzania wako chini ya miaka 40 moja ya changamoto kubwa kwao ni ajira huku sekta pana ya kukuza ajira ni sekta binafsi moja ya njia ya kukuza ajira ni kujua soko hurua ,”amesisitiza Kajula.

Amesema pia watajikita kutoa fursa kubwa kwa wanafunzi waliopo vyuo kwani ujasiriamali ni eneo rahisi ambalo wanaweza kutumia vijana .

“Tunataka nguvu kazi inayokua na yenye uwezo wa kutumia fursa taasisi ya EABC ni muhimu kufanya nchi iende mbele tutatumia zaidi njia za kidigitali katika kuhakikisha ujasiriamali unakua zaidi.

Kajula amesema mkataba huo wa Ushirikiano utakuwa wa miaka mitano ambapo watatoa elimu ya masuala ya fedha jinsi ya kupata mitaji,mikopo,vyanzo vya mapato ambapo watashirikiana na Brela na TRA.

“Ujasiriamali unaanza wazo tunataka kujenga msingi wa uelewa kuna vitu unaweza kufanya bila mtaji tunataka makampuni makubwa yaanzie vyuoni,”amebainisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA,Oscra Kissanga amefafanua kuwa wameingia makubaliano kwasababu wao wanasehemu ya vijana ambao wataweza kusaidiwa kufanya biashara na kupata masoko.

“Tunafanya kazi kwa ukaribu na serikali katika ngazi za Wilaya, Mkoa na Baraza la Taifa na mapendekezo yetu pia yanatumika kutengeneza bajeti ya nchi na kuwasilisha changamoto za wafanyabiashara kunzia ngazi ya chini.

Amesema wanashirikiana na Taasisi zingine kama Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoa elimu ya umuhimu wa kujisajili na kutambulika kisheria.

Habari Zifananazo

Back to top button